YANGA YA ZOA TUZO NNE
Yanga usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kubeba tuzo nne katika utoaji wa zawadi za waliofanya vizuri kwenye msimu uliopita wa Ligi ya Vodacom Tanzania.
Licha ya ubingwa wa taji la Vodacom pia beki Juma Abdul ameshinda
tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa 2015/2016, kwa kumshinda Mohamed
Hussein wa Simba na kiungo wa Mtibwa Sugar Shizza Kichuya.
Mbali na tuzo hiyo, Abdul atajinyakulia kitita cha fedha Sh Milioni
9.2 na hiyo kuwa tuzo yake ya pili kwa msimu uliopita baada ya ile ya
mchezaji bora wa mwezi Machi 2016.
Tuzo nyingine ambayo Yanga wameizoa ni ile ya mfungaji bora ambayo
imechukuliwa na Amissi Tambwe aliyefunga mabao 21 na kuzawadiwa Sh.
Milioni 5.7. Wakati kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe Thabani Michael
Kamusoko anayechezea Yanga pia akishinda tuzo ya mchezaji bora wa
kigeni, na kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 5.7.
Kocha Mdachi Hans van der Pluijm aliiongezea Yanga tuzo ya nne kwa
kuibuka kocha bora wa msimu uliopita na kujinyakulia Sh. Milioni 8
Na zawadi ya tano ambayo ilikuwa inaongozwa kwa ukubwa katika tuzo
zote zilizotolewa na Vodacom ilikuwa ni ile ya ubingwa ambayo
ilichukuliwa na Yanga na kujizolea Sh. Milioni 81.3 kwa kuwa bingwa,
huku Sh. Milioni 40.6 zikienda kwa washindi wa pili, Azam FC, Sh Milioni
29 zikienda kwa washindi wa tatu, Simba SC na Sh. Milioni 23.2 zikienda
kwa Prisons washindi wa nne.
Katika tuzo hizo kipa wa Azam FC, Aishi Salum Manula ameshinda tuzo
ya kipa Bora akiwaangusha Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Benno Kakolanya
wa Prisons.
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Hajib aliibuka mshindi wa tuzo ya goli
bora la msimu na kuzawadiwa Sh. Milioni 3 akimuangusha Tambwe wa Yanga,
wakati Mtibwa Sugar imeibuka timu yenye nidhamu bora na kuzishinda timu
za JKT Ruvu na Mgambo Shooting na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2.
Ngole Mwangole ameshinda tuzo ya Refa Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 baada ya kuwaangusha Anthony Kayombo na Rajab Mrope.
JERRY MURO AACHANA NA SOKA KWA MUDA
"Kila nikizifikiria figisu za soka la bonge aisee nachoka kabisaa, let me walk away for a while though I will be missing my funs and my people wa kimataifa but I must walk away for a while @yangasc"



