Michezo Majuu

  Sunderland ya msajili Moyes

 

Moyes ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Sunderland baada ya aliyekuwa kocha wa Sunderland Sam Allardyce kuchukuliwa na timu ya Taifa ya Uingereza. Moyes amesaini mkataba wa Miaka minne na timu hiyo. Moyes amesema  "Nina furaha sana kujiunga na Sunderland."

 Man U wakubali kumsajili Pogba kwa dau la Euro Mil 110

Man u imekubali kumsajili Paul Pogba kwa dau la kuvunja record ya dunia la Euro milion 110, Maafisa wa Man U wanatarajiwa kukutana na wawakilishi wa Juventus hapo jumatano kukamilisha huo uhamisho.

Pogba anatarajiwa kuvunja rekodi ya dunia kwa uhamisho kwa kumpita Gareth Bale aliyesajili na Real Madrid kutokea Tottenham kwa dau la Euro Million 100.  Pogba anatarajiwa kulipwa Euro Million 13 kwa mwaka na amesema yupo tayari kufanya kazi na Man U.
Man U tayari ishawasajili wachezaji kama Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan and Zlatan Ibrahimovic.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 

Leicester City wanataka pauni milioni 45 kumuuza Riyad Mahrez, 25, lakini wana uhakika kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria atabakia King Power Stadium hasa baada ya kuondoka kwa N'Golo Kante kwenda Chelsea (Telegraph), Manchester United wamechelewesha kutangaza namba za jezi za wachezaji wake kwa msimu mpya mpaka watakapokamilisha usajili wa pauni milioni 105 wa kiungo wa Ufaransa na Juventus, Paul Pogba, 23 (Sun), mwenyekiti wa West Ham, David Sullivan, amesema mshambuliaji Diafra Sakho, 26, haondoki labda timu hiyo ipate mchezaji atakayeweza kuziba pengo lake (Mirror), Arsenal wanapanga kusajili wachezaji wawili kwenye safu ya ulinzi, wakimtaka Jason Denayer, 21 kutoka Manchester City na Matthias Ginter, 22 kutoka Borussia Dortmund (Sun), Bayern Munich na Real Madrid bado wanamfuatilia winga anayesakwa na Manchester City, Leroy Sane, 20, kwa mujibu wa baba wa mchezaji huyo kutoka Ujerumani (Manchester Evening News), dau la Arsenal la pauni milioni 2 limekubaliwa na Bolton la kumsajili beki Rob Holding, 20 (Daily Mail), meneja wa Hull City, Steve Bruce, amekuwa mtu wa pili kufanyiwa usaili wa kuwa meneja wa England, lakini anatarajiwa tu kupewa kazi hiyo iwapo Sam Allardyce hatokubaliana na maslahi yaliyopo (Daily Mail), Barcelona, Real Madrid, Manchester United na Chelsea zimepanda dau la kumtaka kiungo kutoka Ureno anayecheza Valencia, Andre Gomes, 22, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 54 (Mundo Deportivo), Watford wanamfuatilia beki kutoka Ivory Coast Brice Dja Djedje, 25, kutoka Marseille (L'Equipe), Diego Costa, 27, hajaomba kuondoka Chelsea, na mshambuliaji huyo anatarajiwa kusalia Darajani msimu ujao (Evening Standard), meneja wa Chelsea Antonio Conte amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata, 23, akimhakikishia nafasi yake iwapo ataamua kujiunga na Chelsea msimu ujao (Marca), meneja wa Everton Ronald Koeman, anamfuatilia kiungo wa Ureno na Sporting Lisbon William Carvalho, 24 (Mirror), Juventus wanakaribia kuwazidi kete AC Milan katika kumsajili winga kutoka Croatia, Marko Pjaka, 21, ambaye tayari ameaga wachezaji wenzake katika klabu ya Dinamo Zagreb (Gazzetta World), mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Alvaro Negredo, 30, hatosafiri na timu yake ya Valencia kwenda Uholanzi, na badala yake atakwenda England kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Middlesbrough (Gazzetta Live), Marseille wanafikiria kumchukua kwa mkopo mshambuliaji kutoka Cameroon, anayechezea Tottenham, Clinton N'Jie, 22, iwapo winga wao Georges-Kevin N'Koudou atakwenda White Hart Lane (Telegraph). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.